NA K-VIS BLOG, ARUSHA
BENKI Kuu ya Tanzania BoT, imezungumzia uwepo wa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwenye maduka ya kubadilisha fedha za kigeni jijini Arusha.
Taarifa ya Gavana wa BoT iliyopatikana jijini Dar es Salaam leo Jumanne Novemba 20, 2018 imesema, askari wa JWTZ wanaoonekana kwenye maduka ya kubadulisha fedha Bureau de change, wako kwenye zoezi linaloratibiwa na kitengo cha ukaguzi cha BoT na kuongeza kuwa wako kwenye ukahguzi wa kushtukiza.
Taarifa imesema, operesheni hiyo ni ya tatu kufanyikana uchunguzi wa kina katika miezi sita iliyopita ulibaini kuongezeka kwa biashara za kubadilisha fedha za kigeni na utakatishaji wa fedha hususan kupitia maduka hayo ya Bureau de change. Taarifa hiyo iliyosainiwa na Gavana wa BoT, Profesa Luoga imesema.
“Juhudi za kuwapata wahusika hazikuzaa matunda katika operesheni mbili zilizopita kutokana na mtandao mpana na madhubuti wa shughuli hizo ambao na ambao ulilenga kuhakikisha shughuli za udhibiti hazifanikiwi.” Sehemu ya taarifa hiyo in asema.
Kwa sababu hiyo taarifa hiyo inasema, BoT ililazimika kushirikisha vyombo vingi katika kutekeleza zoezi hilo na kwamba hata askari wa JWTZ walioonekana kwenye maduka hayo walikuwa hawana silaha na kwamba ilikusudiwa kuongeza umakini na usalama katika kutekeleza operesheni hiyo.
Taarifa hiyo inawashukuru wakazi wa jiji la Arusha kwa kuwa watulivu wakati wa operesheni hiyo na kwamba mahojiano na watu waliokamatwa yameanza na ikibainika walikwenda kinyume cha sheria watachukuliwa hatuia kali ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa leseni zao. Taarifa kamili ya BoT inapatikana hapo chiuni

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇