Serikali ya Kenya imeamua kujiimarisha kwa kudhibiti mipaka yake ya majini ambayo imekuwa ikitumiwa vibaya na makundi ya wahalifu hususan magendo ya madawa ya kulevya na binaadamu.
Hatua hiyo imefikiwa kufuatia Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo kuasisi kikosi kazi ambacho kitasimamia ulinzi katika mipaka ya baharini ikiwemo kukabiliana na wavamizi wanaotokea nchi jirani.
Hii ni baada ya serikali ya Nairobi kulalamika kwa mara kadhaa juu ya kuporwa raslimali zake za baharini wakiwemo samaki ambapo meli za kigeni bila kuwa na kibali kutoka mamlaka husika za nchi hiyo.
Kwa maelezo zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa, Seifullah Murtadha…………./
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇