LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 21, 2018

MAZUNGUMZO YA WAZIRI WA MASHAURI YA KIGENI WA UINGEREZA MJINI TEHRAN; UKOSOAJI WA IRAN KWA UMOJA WA ULAYA

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran jana Jumatatu alisema katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Jeremy Hunt, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza kwamba, kukiukwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA maana yake ni kukanyagwa na Marekani hadhi, heshima na nafasi ya kisiasa ya Umoja wa Ulaya.
Ali Shamkhani ameikosoa pia serikali yya Uingereza kutokana na hatua yake ya kuziuzia silaha na zana za kijeshi nchi zinazokiuka na kukanyaga haki za binadamu kama Saudi Arabia na Bahrain. Shamkhani amesisitiza kuwa, hatua yoyote ya baadhi ya nchi za Ulaya ya kuwa pamoja na siasa za serikali ya Marekani itapelekea kuibuka mtazamo hasi kwa nchi hizo mbele ya fikra za waliowengi za taifa la Iran na mataifa ya Mashariki ya Kati na kuonekana kuwa washirika wa jinai za Marekani, utawala haramu wa Israel na madola ya Mashariki ya Kati yenye fikra mgando.
Tangu Marekani ijiondoe katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, madola ya Ulaya kutokana na sababu mbalimbali yamekuwa yakisisitiza juu ya kuweko ushirikiano kati yao na Iran hususan katika masuala ya biashara na uchumi. Hata hivyo, misimamo ya madola hayo ya Ulaya dhidi ya ukwamishaji mambo wa Marekani katika utekelezwaji wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA imekuwa ikiishia katika kutoa taarifa tu.
Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran (kulia) alipofanya mazungumzo na Jeremy Hunt, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza
Mmoja wa wachambuuzi mahiri wa masuala ya kisiasa wa Kanali ya televisheni ya France-24 anasema: Licha ya kuwa sheria za Ulaya zina mipaka mno na dhaifu mkabala na Washington, lakini nchi hizo haziwezi tena kuivumilia Marekani na kuiona ikiwa polisi ya dunia.
Filihali, maamuzi ya Ulaya yanachukuliwa kwa mwendo wa kinyonga. Umoja wa Ulaya una njia mbili mbele yake. Mosi, ichukue maamuzi kwa kujitegemea na kwa mamlaka ili kuonyesha kuwa, umoja huo unafungamana na mikataba ya kimataiifa. Njia ya pili ni kusalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani na bila shaka mwenendo huo hautaishia tu katika suala la makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwani katika mustakabali uamuzi huo utaigharimu pakuba Ulaya.
Ukweli wa mambo ni kuwa, vikwazo vya Marekani ni kinyume cha hati ya Umoja wa Mataifa, haki za binadamu na kinyume kabisa na maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Vikwazo hivyo vinawalenga wananchi wa Iran moja kwa moja na chelewa chelewa na hatua yoyote ya Ulaya ya kusitasita mkabala na ukiukaji huu wa sheria wa Marekani itakuwa na madhara kwa mataifa yote ya dunia.
Pande zilizosalia katika JCPOA baada ya Marekani kujiondoa
Msimamo wa Umoja wa Ulaya kwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hauwezi kutathminiwa kuwa, uungaji mkono thabiti na imara kwa makubaliano fulani katika fremu ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Pengine katika mtazamo mzuri kabisa inawezekana kusema kuwa, hadi sasa misimamo ya Umoja wa Ulaya kuhusiana na makubaliano ya JCPOA ingali imetawaliwa na utata na hali ya shaka.
Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano na gazeti la The Guardian la Uingereza, Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sanjari na kuonyesha kutoridhishwa kwake na mwenendo wa kinyonga wa Umoja wa Ulaya katika kuanzisha mfumo maalumu wa ubadilishanaji fedha unaojulikana kama SPV alisema:  Kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Ulaya imetoa ahadi ya kisiasa lakini inasikitisha kwamba, kivitendo imekuwa ikifanya mambo kwa mwendo wa kinyonga sana.
Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya
Ni jambo lisilo na shaka kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuzingatia hatua za kusitasita za upande wa pili mkabala na hatua zisizofaa za Marekani, imeazimia kuchukua maamuzi ya lazima kulingana na maslahi yake ya kitaifa na majukumu yake. Matamshi ya Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran katika uwanja huu yako bayana na wadhiha kabisa. Akizungumza jana Jumatatu katika Kongamano la Kimataifa la Mfumo wa Kimataifa Abbas Araqchi alisema: Nchi za Ulaya na nchi nyingine husika katika makubaliano ya JCPOA kama zinataka kulinda itibari na heshima yao kimataifa, zinapaswa kuandaa mazingira ya kudhamini maslahi ya Iran katika makubaliano hayo.
Endapo makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yatakabiliwa na tatizo, usalama wa Ulaya nao utakabiliwa na matatizo, na kama Marekani inafikiria kuwa, Mashariki ya Kati isiyo na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA itakuwa salama zaidi, basi bila shaka inakosea mno.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages