LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2018

HATIMA YA WATOTO WALIOPOTEZANA NA WAZAZI WAO MASHAKANI HUKO KASAI DRC

Mashirika ya kutetea haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanasema kuwa, mamia ya watoto ambao walikuwa sehemu ya raia wa nchi hiyo waliofukuzwa kutoka Angola, hawana makazi na wanazurura tu katika jimbo la Kasai.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, hali hiyo imetokana na madhara ya kufukuzwa kwa nguvu na mamlaka nchini Angola, ambazo zinatuhumiwa kuendesha operesheni hiyo bila kuzingatia haki za binadamu.
Taarifa za mashirika hayo zinasema kuwa, watoto hao ambao wana umri wa kati ya miaka 4 hadi 12 ni wale ambao baada ya kufukuzwa Angola, walipotezana na wazazi wao na hivi sasa hawana pa kwenda.
Kwa mujibu wa Babar Baloch msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ni kuwa, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walilazimishwa kuvuka mpaka na kurudi kwao baada ya kufukuzwa kutoka Angola.
Wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokkrasia ya Congo
Uamuzi huo ulitokana na hatua ya serikali ya Angola ya kuwafukuza wahamiaji wa DRC, ambao inasema wengi wao walikuwa wakifanya kazi katika sekta isiyo rasmi ya madini katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kushughulia tatizo la watoto hao waliopotezana na wazazi wao.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesisitiza kuwa, itaichukulia hatua za kimataifa nchi ya Angola kutokana na kuwafukuza raia wake kwa nguvu huku kukiwemo na ripoti kwamba, walifanyiwa vitendo vya unyama na ukatili wakati wa kufukuzwa nchini humo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages