Waziri Mkuu wa Malaysia, Mahathir Mohamad amesema taifa lake halitakubali mashinikizo ya kuruhusu na kuheshimu eti haki za mashoga, wasagaji na watu waliobadilisha jinsia zao pamoja na ndoa za watu wa jinsia moja.
Akihutubu hii leo katika Chuo Kikuu cha Chulalongkorn mjini Bangkok nchini Thailand ikiwa ni katika siku ya pili ya ziara yake nchini humo, Dakta Mahathir Mohamad amesema, "Sisi (Malaysia) hatukubaliana na uozo huo wa mahusiano na ndoa za watu wa jinsia moja, iwapo (Wamagharibi) wanaunga mkono ufuska huo, hilo halituhusu. Msitulazimishe. Iwapo watatembea uchi, je tunapaswa kuwafuata pia?"
Waziri Mkuu wa Malaysia amesema hii leo nchi za Magharibi hazithamini masuala ya ndoa na familia kuhoji, je kuna lazima gani watu wengine wawaige?
Amesisitiza kuwa ufuska huo ni katika thamani na tamaduni za Kimagharibi na nchi yake haitakubali kutwishwa uozo huo wa kijamii.
Dakta Mahathir Mohamad amebainisha kuwa, Malaysia ambayo asilimia 60 ya jamii yake ni Waislamu, inaheshimu na itaendelea kuheshimu utamaduni na taasisi ya ndoa na familia.
Amesema inashagaza namna Wamagharibi katika zama hizi wanaona ni jambo la kawaida wanaume kuwaoa wanaume wenzao na wanawake kuwaoa wanawake wenzao, lakini wanakimbia kukodi watoto ili familia zao zionekane zimekamilika. Ameongeza kuwa, Malaysia katu haiwezi kukumbatia ufuska huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇