JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI - HUDUMA ZA AFYA ZAENDELEA KUBORESHWA
17.9.2018
Ndugu zangu:
(1) Wananchi ndani ya VIJIJI kadhaa wanaendelea na UJENZI WA ZAHANATI ZA VIJIJI VYAO.
(2) WADAU WA AFYA wameendelea kutoa MICHANGO YAO, k.m. (a) Maabara ya Kituo cha Afya Murangi inaboreshwa kwa Tsh Milioni 15, (b) Kiliniki ya VVU inajengwa Murangi, Tsh Milioni 30 na (c) Kliniki ya VVU inajengwa Bukima, Tsh Milioni 30.
(3) BAJETI YA SERIKALI
(a) Hospital ya Wilaya itajengwa Kwikonero, Kijijini Suguti. Tsh Bilioni 1.5
(b) Zahanati ya Mugango kupanuliwa kuwa KITUO CHA AFYA. Serikali imetoa Tsh Milioni 400. Matayarisho yamekamilika ujenzi karibu unaanza...OMBI KWAKO...
UJUMBE KUTOKA KWA DMO:
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imepokea kiasi cha Tshs milioni 400 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi/ukarabati wa Kituo cha Afya Mugango. Majengo yaliyopendekezwa kujengwa ni kama ifuatavyo;
(i) Jengo la Mama na Mtoto
(ii) Jengo la Upasuaji
(iii) Jengo la Maabara
(iv) Jengo la Kuhifadhia Maiti (Mortuary), na
(v) Nyumba ya Mtumishi
Ili kukamilisha ujenzi huu inatakiwa iongezeke kiasi cha Tsh Milioni 38 na mwisho wa kukamilisha ujenzi huu ni Tarehe 30 Novemba 2018
Ndugu zangu:
Tunaomba MCHANGO wako ili kukamilisha UJENZI HUU KAMA ILIVYOPANGWA. Mbunge Prof Sospeter Muhongo alishachangia SARUJI MIFUKO 400.
MCHANGO WAKO UTAPOKELEWA na DC (Wilaya ya Musoma), DED (Halmashauri) au DIWANI WA KATA YA MUGANGO.
TUSHIRIKIANE NA SERIKALI YETU KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA MUGANGO kabla ya Tarehe 30.11.2018
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Your Ad Spot
Sep 17, 2018
Home
Unlabelled
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇