Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akiongozana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege TAA Bw. Richard Mayongela wakati alipotembelea eneo ambalo wahanga wa upanuzi wa uwanja wa Ndege wa JNIA wa jijini Dar es salaam wanatakiwa kupatiwa viwanja vipya.
Mwakilishi wa kampuni ya Remix Tanzania Limited BwLwembo Henjewele akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati alipotembelea katika mradi wa viwanja vitakavyogawiwa kwa wananchi walioathirika na upanuzi wa uanja wa Ndege wa JNIA.
Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiyeakiangalia moja ya nyaraka za mkataba wa wananchi hao na kampuni ya Remix Tanzania Limited ambao kampuni hiyo haijatekelezwa mpaka sasa.
Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege TAA Bw. Richard Mayongela kulia wakati alipotembelea eneo ambalo wahanga wa upanuzi wa uwanja wa Ndege wa JNIA wa jijini Dar es salaam wanatakiwa kupatiwa viwanja.
……………………………………………………………………..
Tanzania Remix wamejipatia fedha kiasi cha bilioni 3.7 fedha za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) ambazo zilikuwa kwa ajili ya fidia kwa wahanga wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya kununua maeneo ya wananchi waliokuwa wananishi kipunguni A na Kipunguni Mashariki.
Akizungumza na wanachi wa kata ya Luhangwa Kata ya Msongola manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam leo, Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea viwanja vya fidia vya Luhangwa amesema kuwa serikali inataka viwanja ambavyo havina mgogoro na vilivyolipiwa kwa kuwa serikali ilishalipia fedha viwanja vyote 537 ambavyo vina thamani ya shilingi bilioni 3.7.
” Tanzania Remix ninawapa wiki moja kupima na kuwalipa wananchi fedha zao za viwanja kulingana na mkataba wao na nyinyi . Msipofanya hivyo Jumatatu ya Septemba 24,2018 hamtarudi nyumbani mtaenda sehemu tofauti na nyumbani ” Amesema Nditiye.
“Tanzania Remix imelipwa Fedha ya viwanja 537 ambavyo vinatakiwa kugawiwa kwa wananchi wa kipungunj A na Kipunguni Mashariki kama fidia yao kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege na kwakuwa hawajawalipa wenye vinjwa leo tuahirishe shughuli ya ukaguzi wa viwanja na tuwape muda Tanzania Remix kuwalipa wenye viwanja kwa kadili ya walivyosaini mkataba”.
Nditiye ameiagiza Tanzania Remix ifikapo Septemba 24 mwaka huu iwalipe fedha wananchi atakagua viwanja visivyo na mgogoro na wananchi vilivyopangiliwa vizuri kila kiwanja kikijitegemea na vyenye barabara zinazoeleweka.
Mwenyekiti wa mtaa wa Luhangwa, Salum Kipendo amesema kuwa yeye pamoja na anaowaongoza hawajalipwa fedha za viwanja kadiri ya mkataba unavyosema asilimia 40 Tanzania Remix na wananchi asilimia asilimia 60.
Nae Mrisho Hashimu mmiliki wa shamba amesema kuwa yeye na baadhi ya wenzake hawajalipwa fedha za ununuzi wa viwanja kadili ya mkataba waliosaini wao na Tanzania Remix tangu mwaka 2014 kwa ajili ya viwanja vya wananchi waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇