Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndugu Hassan Bomboko amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja wa Vijana Jazz Band Ndugu James Rock Mwakibinga.
Ndugu Bomboko akiwa Ofisini kwake, Ofisi ndogo za UVCCM Makao Makuu zilizopo Upanga Jijini Dar Es Salaam amemkabidhi vitendea kazi na mpango mkakati.
"Ndugu Mwakibinga unayo nafasi ya kuonyesha maarifa, uwezo na uweledi wako kwa vitendo, umeaminika UVCCM na kupewa dhamana ya kuwa msimamizi wa Bendi ya Vijana nenda katumie vipawa vyako kwa maslahi mapana ya Jumuiya yetu ya Vijana wa CCM, Chama Cha Mapinduzi na Nchi yetu kwa ujumla" alisema Ndugu Hassan Bomboko.
Aidha, Katibu Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Ndugu Khamana Simba naye ameungana na Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi kwenye ukaribisho huo na amemjuza Ndugu Mwakibinga kuwa kuna Vijana wengi wa Vyuo na Vyuo Vikuu nchini wenye vipaji lukuki hivyo anayo nafasi ya kuwaona na kuwatumia wazalendo hao kwenye shughuli za Bendi ya Jumuiya, Vijana Jazz Band.
Your Ad Spot
Sep 17, 2018
Home
Unlabelled
MWAKIBINGA AKABIDHIWA VITENDEA KAZI NA MPANGO MKAKATI KATIKA KUISUKA UPYA VIJANA JAZZ BAND
MWAKIBINGA AKABIDHIWA VITENDEA KAZI NA MPANGO MKAKATI KATIKA KUISUKA UPYA VIJANA JAZZ BAND
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇