Rais Azali Assoumani wa Comoro ameshinda kura ya maoni ya kurefusha kipindi cha uongozi wa rais na kukomesha mfumo wa kuongoza kwa zamu baina ya visiwa vitatu vikuu vinavyounda Jamhuri ya watu wa Comoro.
Assoumani amesema asilimia 92.74 ya Wacomoro wamepiga kura ya ndiyo ya kufanyiwa mabadiliko kipengee cha katiba kinachuhusu muhura wa rais na asilimia 7.26 wamepinga mabadiliko hayo.
Kura hiyo ya maoni sasa inamruhusu Azali Assoumani kugombea tena kwa vipindi vingine viwili vya miaka mitano mitano kuanzia uchaguzi uliopangwa kufanyika mapema mwakani badala ya kuondoka madarakani baada ya kipindi chake cha sasa kumalizika mwaka 2021.
Rais Azali Assoumani wa Comoro anasema mfumo wa kupokezana madaraka unatatiza kuweka mipango na vipaumbele vya muda mrefu kwa ajili ya kuongoza nchi.
Kambi ya upinzani imepinga zoezi la kura ya maoni lililofanyika tarehe 30 Julai na kumtuhumu Rais Asoumani kuwa amekiuka katiba. Kiongozi huyo amesitisha Mya Katiba, na sasa upinzani unasema kura ya maoni ya kipindi cha rais haiwezi kuwa halali mpaka pale mahakama hiyo itakaporejeshwa.
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuheshimiwa katiba na kuzitaka pande zote kuanza mazungumzo haraka iwezekanavyo.
Katiba ya sasa ya Comoco inaamuru kuwa nafasi ya rais inapaswa kuchukuliwa kwa zamu na kwa kupokezana baina ya viongozi wa visiwa vitatu vikuu vya nchi hiyo ambavyo ni Ngazidja Mohéli na Anjouan.
Azali Assoumani anajiunga na viongozi kadhaa wa nchi za Afrika kama Rwanda, Uganda na Cameroon waliorefusha kipindi cha uongozi wa rais au kubadilisha katiba kwa shabaha ya kubakia madarakani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇