Gazeti la Washington Post la nchini Marekani limeripoti kuwa, Donald Trump ndiye Rais mwongo zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Gazeti hilo limeandika katika toleo lake la leo Alkhamisi kwamba, katika kipindi cha siku 558 zilizopita, Rais Donald Trump wa nchi hiyo amesema uwongo au kutoa matamshi yasiyo sahihi mara 4229.
Gazeti hilo limeendelea kueleza kwamba, kwa mujibu wa ripoti zilizopo ni kuwa, katika kipindi cha miezi miwili pekee iliyopita, Rais Donald Trump amesema au kutoa madai ya urongo mara 978.
Gazeti hilo limeendelea kueleza kwamba, kwa mujibu wa ripoti zilizopo ni kuwa, katika kipindi cha miezi miwili pekee iliyopita, Rais Donald Trump amesema au kutoa madai ya urongo mara 978.
Ripoti iliyochapishwa na gazeti hilo la Washington Post inabainisha kwamba, katika mwaka wa kwanza wa kuwa kwake katika Ikulu ya Rais ya White House, Trump amesema uongo au kutoa matamshi ya upotoshaji mara 2140 na kwamba, takwimu hizo ziliongezeka maradufu katika kipindi cha miezi sita baadaye.
"Katika masuala yanayohusiana na biashara ya kimataifa, Trump alitoa matamshi yasiyo sahihi na ya upotoshaji mara 432", imeendelea kubainisha ripoti hiyo.
Kuhusiana na siasa za kigeni za Marekani, hususan gharama za Shirika la Kijeshi la NATO, Rais Dionald Trump ametoa matamshi ya uwongo mara chungu nzima.
Wachambuzi wa mambo wamekuwa wakimkosoa Donald Trump ambaye amekuwa akiropoka mara kwa mara kuhusiana na masuala mbalimbali wakisema kuwa, bwabwaja zake zinashusha hadhi ya cheo cha Rais nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇