Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani Prof. Matthew Sackett akiwaelekeza Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kumuwekea mgonjwa kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Implantable cardioverter defibrillator - ICD) katika kambi maalum ya siku saba ya matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakiandaa vifaa vitakavyotumika katika upasuaji mdogo wa kumuwekea mgonjwa kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Implantable cardioverter defibrillator - ICD) katika kambi ya matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo.
Picha na Genofeva Matemu - JKCI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇