Duru za habari nchini Yemen zimetangaza kwamba, idadi ya watu waliopoteza maisha katika shambulizi la ndege za muungano vamizi wa Saudi Arabia dhidi ya hospitali ya 'al-Thawrah' ya mji wa Al Hudaydah, magharibi mwa Yemen, imefikia watu 52.
Aidha kwa mujibu wa habari hiyo, watu wengine 70 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo la kinyama. Awali duru za habari zilikuwa zimetangaza kwamba katika hujuma hiyo ni watu 26 waliopoteza maisha na wengine 35 kujeruhiwa. Jioni ya jana ndege za kivita za muungano vamizi wa Saudia ziliishambulia kwa makombora hospitali ya al-Thawrah katika mkoa Al Hudaydah. Hii sio mara ya kwanza kwa ndege za kijeshi za muungano huo, kufanya hujuma na mauaji dhidi ya asasi za kijamii na kiraia nchini Yemen, tena mbele ya macho ya walimwengu.
Ni kutokana na hali hiyo ndipo hivi karibuni Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF, ukautaka utawala wa Aal-Saud, ukomeshe mashambulizi yake dhidi ya miundombinu ya Yemen. UNICEF, ilitoa taarifa hiyo Jumatano iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine iliutaka muungano huo vamizi unaoongozwa na Saudia, ukomeshe mashambulizi yake dhidi ya miundombinu ya msingi ya Wayemen, hususan kwenye vyanzo vya maji vya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇