Serikali ya Congo imemzuia Gavana huyo zamani wa jimbo la Katanga anayeishi uhamishoni Afrika kusini kurudi nyumbani.
Katumbi aliomba ruhusa kuingia nchini leo asubuhi kuwahi kuwasilisha makaratasi yake ya uteuzi wa chama kuwa mgombea urais kwa tume ya uchaguzi nchini.
Maafisa wa polisi huko Lubumbashi wameweka vizuizi katika bara bara kuu na usalama umeimarishwa ndani na katika maeneo yalio karibu na uwanja wa ndege.
Kuna mipango ya kuzifunga njia za ndege kutua kuizuia ndege ya Katumbi isitue DRC.
Moise Katumbi ni nani?- Jina lake la mwisho pia Tshapwe
- Anajulikana kama Moses Katumbi nchini Zambia, ambapo aliishi kwa miaka mingi
- Tarehe ya kuzaliwa 28 Disemba 1964
- Eneo la kuzaliwa ni Kashobwe
- Ni kabila la Babemba
- Ni kaka wa kambo wa Katebe Katoto, maarufu kama Rafael Soriano, na mfuasi wa Laurent Nkunda
- Baba yake ni Padre Nissim Soriano, Mitaliano Myahudi kutoka Rhodes
- Mama yake ni Virginie Katumbi, kutoka familia ya kifalme ya Kazembe
- Rais wa kalbu ya Soka TP Mazembe Football iliopo Lubumbashi
- Anajullikana kwa mapenzi yake na kofia za mtindo 'Cowboy'
Waziri wa habari Lambert Mende anasema gavana huyo wa zamani kutoka jimbo lenye utajiri mkubwa wa madini atakamatwa iwapo atajaribu kuingia nchini kwa ndege ya usafiri wa abiria.
Katumbi aliondoka nchini Congo mnamo 2016 baada ya kukosana na rais Joseph Kabila.
Baadaye alishtakiwa kwa udanganyifu wa mali na alihukumiwa miaka mitatu gerezani pasi yeye kuwepo mahakamani.
Kiongozi mwingine wa upinzani - Jean-Pierre Bemba - alirudi DRC siku ya Jumatano baada ya kutokuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja.
Aliwasilisha makaratasi yake ya kugombea urais hapo jana Alhamisi.
" Ninaweza kuthibitisha kuwa nilikuwa na kadi ya kupiga kura, na nimewasilisha nyaraka zote," shirika la habari AFP linamnukuu Bemba akizungumza nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi.
Hatahivyo chama tawala kimesema hafai kugombea kutoana na kushtakiwa kwa rushwa katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC. Amekataa rufaa kupinga kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇