Habari kutoka Syria zinaarifu kwamba kikosi cha ulinzi wa anga cha nchi hiyo kimetungua makombora matatu na ndege mbili zisizo na rubani za utawala haramu wa Kizayuni katika viunga vya mji wa Damascus.
Kwa mujibu wa habari hiyo, awali kikosi hicho cha ulinzi wa anga kilitungua makombora mawili kusini mwa mji wa Damascus, mji mkuu wa Syria huku kombora jingine likisambaratishwa kaskazini magharibi mwa mji huo. Aidha imeongeza kwamba kikosi hicho kimefanikiwa kuzinasa na kuzitungua ndege mbili zisizo na rubani za kijasusi za utawala wa Kizayuni, magharibi mwa mji huo. Katika wiki za hivi karibuni Israel, imekithirisha mashambulizi yake nchini Syria.
Hii ni kwa kuwa utawala huo pandikizi una wasi wasi wa kushindwa makundi ya kigaidi. Mgogoro wa Syria uliibuka mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Saudia, Marekani, Israel na washirika wao ndani na nje ya eneo kuyatuma makundi hayo kwa lengo la kuleta mabadiliko ya mlingano katika eneo la Mashariki ya Kati kwa maslahi ya Israel. Hata hivyo njama hizo zimeshindwa kufikia malengo yake kutokana na ushindi wa jeshi la Syria kwa msaada wa washauri wa kijeshi wa Iran na uungaji mkono wa Russia dhidi ya magaidi wa Daesh (ISIS). Aidha makundi mengine ya kigaidi nayo yanaendelea kushindwa katika uwanja wa vita, suala lililoitia wasi wasi mkubwa Israel.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇