Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza na kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale.
NA K-VIS BLOG
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameamuru Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kuchukua umiliki wa viwanja namba 1 na namba 13 kitalu namba 46 vinavyotumiwa na wachonga vinyago na wafanyabiashara ya vinyago pale Mwenge jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mwakyembe ametoa uamuzi huo leo Agosti 20, 2018 kutokana na utata mkubwa wa nani hasa mmiliki halali wa eneo hilo, ambapo mgogoro huo umedumu kwa takriban miaka 33, bila kupatiwa ufumbuzi, alisema.
“Mgogoro huu unaweza kabisa ukaendelea kudumu kwa miaka mingine 33 kutokana na mgawanyiko mkubwa uliopo kati ya wachonga vinyago na wafanyabiashara ya vinyago, lamsingi tumesema wote wawili wasipewe umiliki.” Alisema na kuongeza.
“Msimamo wa Serikali, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeona njia pekee ya kuishi dhamira ya awali ya serikali ya kuendeleza sanaa ni kuhamisha umiliki wa viwanja hivyo viwili kutoka Makonde, kwenda Baraza la Sanaa la Taifa BASATA.” Alifafanua.
Akifafanua kuhusu utaratibu mpya sasa Dkt. Mwakyembe alisema, BASATA ihakikishe mambo matatu kufanyika ambayo ni kuhakikisha wachonga vinyago na wafanyabiashara ya sanaa 56 waliohamishwa kutoka Barabara ya Bagamoyo na Sky Way Hotel na kuhamishiwa pale Mwenge, BASATA ihakikishe wanapewa fursa sawa ya kuimarisha na kuendeleza sanaa za ufundi na soko lake.
Aidha wale wote walionunua vibanda kutoka kwa wahamishiwa wa mwanzo na wengine kati ya mwaka 1984 na leo BASATA ihakikishea wanahakikiwa na kueleweshwa kuwa walinunua vibanda na sio ardhi, ardhi inamwenyewe.
Agizo lingine alilotoa Dkt. Mwakyembe kwa BASATA ni kuhakikisha kuwa kuendesha biashara nyingine yoyote mbali na sanaa za ufundi ndani ya viwanja hivyo ni kupoteza uhalali wao wa kuwepo hapo.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na wasanii wa kuchonga vinyago (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA) Geofrey Mngereza na kulia ni Rais wa Shirikisho la Sanaa za Uchongaji, Adrian Nyangamale.
Baadhi ya wasanii wa sanaa za uchongaji wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 33 katika eneo la vinyago Mwenge.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇