Na Mathias Canal-WK,
Bukoba-Kagera
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt
Charles Tizeba (Mb) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe
Charles Mwijage wamewasili Mkoa Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku
tatu kuanzia 10 Julai 2018 hadi 13 Julai 2018.
Ziara hiyo imeanza kwa mawaziri
hao kupokea taarifa Mkoa huo iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Mustapher Kijuu kuhusu sekta ya Kilimo na sekta ya viwanda,
biashara Uwekezaji.
Katika ziara hiyo kwa pamoja
watakutana na wadau wa kahawa, kutembelea Chama cha msingi Kwarukwazi Wilayani
Kyerwa, sambamba na kukutana na wadau wa Kahawa na viwanda vinavyokoboa Kahawa
Wilayani Karagwe.
Katika siku ya pili ya ziara
hiyo mawaziri hao watatembelea na kuongea na uongozi wa viwanda cha Sukari
Kagera, kukutana na wadau wa Kahawa na kutembelea Chama cha msingi cha Kyaka
Wilayani Misenyi.
Tarehe 11 Julai 2018 ikiwa ni
siku ya tatu ya ziara hiyo mawaziri hao kwa pamoja watakutana na wadau wa
Kahawa na kutembelea Chama cha msingi Izigo Wilayani Muleba.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇