LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 11, 2018

NAIBU WAZIRI WA NISHATI, SUBIRA MGALU AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI REAIII WILAYANI KILOSA, VIJIJI 180 MKOANI MOROGORO KUNUFAIKA

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, na viongozi wengine wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini REA Awamu ya Tatu (REAIII), kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro Julai 9, 2018. Mhe. Naibu Waziri pia alitumia fursa hiyo kusikilzia kero za wnanchi kuhusu upatikanaji umeme kwenye vijiji vyao.


NA K-VIS BLOG, MOROGORO

NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, amezindua mradi wa usambazaji umeme vijini REA awamu ya tatu (REAIII), ambapo jumla ya vijiji 180 vya Mkoa wa Morogoro vitanufaika.
Naibu Waziri alifanya uzinduzi huo kwenye kijiji cha Mandera Wilayani Kilosa Mkoani humo Jumatatu Julai 9, 2018 kwa kukata utepe na kuwasha swichi ya umeme na hivyo kuibua shangwe, nderemo na vifijo kutoka kwa wananchi waliojawa na furaha.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo Mhe. Naibu Waziri Subira Mgalu, alisema, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli inayo dhamira ya kweli ya kuhakikisha ahadi zote ilizotoa kuhusu upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wote wa Tanzania mijini na vijijini inatekelezwa kwa kasi.
“Tayari umeme umefika sasa utumieni kika milifu kujiletea maendeleo yenu na taifa kwa ujumla.” Alisema Mhe. Naibu Waziri.
Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni nafuu sana kiasi cha shilinbgi Elfu Ishoirini na Saba tu (27,000) 

 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa wakati wa ziara yake kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi kuhusiana na mradi wa umeme vijijini (REA) REA Awamu ya Tatu (REAIII) mzunguko wa tatu mkoa wa Morogoro.
 Wananchi wakimsikilzia Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakayti akihutubia
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mafulu kata ya Kitete wilaya ya Kilosa
 Diwani wa kata ya Kimamba A, Upendo Mpoto akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu wakati akisikiliza kero zinazohusiana na mradi wa umeme vijijijini.
Diwani wa Kata ya Kimamba akizungumza kwenye mkutano huo.
  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (Mwenye Kilemba chekundu kichwani) akimsikiliza Diwani wa kata ya Kitete wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Bw. Stephen Lukobe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Maful. Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Maganga.


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu kulia akizungumza jambo na Diwani wa kata ya Kitete wilaya ya Kilosa, Stephen Lukobe katika ofisi ya kijiji cha Madudu wakati wa ziara ya naibu waziri huyo ya kutembelea vijiji vitavyonufaika na mradi wa umeme wa REA Awamu ya tatu (REAIII), mzunguko wa tatu mkoa wa Morogoro Julai 9, 2018
Makzi wa kijiji cha Mandera, Wilayani Kilosa, akizungumza mbele ya Naibu Waziri

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages