LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 30, 2018

WAZIRI AMINA SALUM ALI AIPONGEZA DHL KWA KUWANOA WAJASIRIAMALI WA ZANZIBAR KUHUSU NAMNA WANAVYOWEZA KULIFIKIA SOKO LA KIMATAIFA KIDIGITALI

 Waziri wa Biashara na Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Amina Salum Ali, akipeana mikono na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Kimataifa ya kusafirisha mizigo na vifurushi DHL, Bw. Paul Makolosi, wakati wa uzinduzi wa semina ya mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu namna ya kulifikia soko la Kimataifa kidigitali. Semina hiyo iliyowaleta pamoja wajasiriamali kutoka Pemba na Unguja ilifanyika mjini Unguja.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Amina Salum Ali, amepongeza hatua ya kampuni ya Kimataifa ya kusafirisha vifurushi ya DHL, kwa kuendesha semina kwa wajasiriamali wa Unguja na Pemba kuhusu fursa mpya ya kulifikia soko la Kimataifa kidigitali.Mhe. Waziri ametoa pongezi hizo wakati akifungua semina hiyo iliyofanyika mjini Unguja, na kuwaleta pamoja wajasiriamali kutoka visiwa vya Unguja na Pemba, ambapo Wataalamu wa DHL, walitoa elimu ya namna ya kutumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zao na DHL kama kampuni inayojishuhghulisha na utoaji huduma za kimataifa za usafirishaji itakuwa rahisi kupeleka bidhaa zao kwa walaji popote pale Duniani.
“Bidhaa za Zanzibar zinapendwa na sisi tunaona kuwa zinaweza kuuzika katika soko la Kimataifa hivyo tuliona jambo la kwanza tupate chombo cha kusafirisha maana mtu anapoagiza bidhaa zake azipate katika kipindi cha wiki moja au mbili hivyo tukaona DHL kwa kuwa ni kampuni inayojulikana Duniani na yenye uzoefu mkubwa wa kupeleka mizigo kwa haraka, tukaona tuwaite ili watoe mafunzo kwa wajasiriamali wetu.” Alisema Mhe. Waziri Amina Salum Ali.
Alisema biashara mtandao sio jambo gumu sana maana watu wengi hivi sasa wanazo smart phone hivyo kupitia simu zao wanaweza kuwasiliana na wateja mbalimbali kupitia kwa kutangaza bidhaa zao kwenye, Instagram na YouTube na kasha mteja anapohitaji DHL wanamfikishia mara moja huko aliko.
Kwa upande wake, Meneja  Mkazi wa DHL, hapa nchini, Bw.Paul Makolosi, alisema, Semina hiyo ni moja ya mipango ya jinsi ya kuwashauri wauzaji na wafanyabiashara kupata mbinu za kuimarisha  uwezo wa usafirishaji wa bidhaa na jinsi ya kuvutia wanunuzi Kimataifa kupitia mitandao ya kijamii.
“Biashara za kimataifa kupitia mtandao zinakuwa kwa kasi kubwa sana, na tunataka wateja wetu wakamate fursa ya hilo soko kwa kuongeza thamani ya bidhaa zao na ndio maana leo tuko hapa kutoa elimu kwa wateja wetu.” Alisema Bw. Makolosi.
Alisema wafanyabiashara wa Zanzibar, wanaweza kuboresha bidhaa zao na kuziweka kwenye mitandao kwa njia ya picha, na kisha mteja anapovutiwa na bidhaa hiyo wanaeweza kuitumia DHL kufikisha bidhaa hiyo kwa mteja popote pale Duniani ambapo DHL inao mtandao mpana wa usafirishaji ikiwa na jumla ya ndege 250 na washirika wengine(Mashirika ya dnege).Kaulimbiu ya semina hiyo ni “Tunataka kupeleka bidhaa za Zanzibar Duniani.”
 Mhe. Amina Salum Ali
 Mhe. Amina Salum Ali, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo.
 Mhe. Amina Salum Ali, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo.
 Baadhi ya washiriki wa semina
 Baadhi ya washiriki wa semina
 Bw. Paul Makolosi, Meneja Mkazi wa DHL Express hapa nchini, akionyesha simu aina ya Smartphone, kuwa ndio kitendea kazi muhimu katika biashara ya kisasa ya kidigitali
 Mwakilishin kutoka kampuni ya Omary Packaging, wanaojihusisha na utengenezaji wa stika na vifungashio, akitoa mmada kuhusu namna ya kuboresha muonekano wa bidhaa kupitia stika na vifungashio bora.




 Mtaalamu kutoka DHL, Venessa Dewing akitoa mada
 Mtaalamu kutoka DHL, Venessa Dewing akijibu maswali
 Bw. Paul Makolosi, akijibu baadhi ya hoja za wanasemina

 Bw. Makolosi, akizungumza na baadhi ya wajasiriamali


 Bi. Sophia Mhando, mmoja wa wafanyabiashara wa kati ambaye hutumia DHL kusafirisha bidhaa zake nje ya nchi, akitoa ushuhuda wa jinsi ambavyo amekuwa akifanikiwa kufanya biashara kupitia mtandao
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo.

 Mhe. Waziri Amina akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa DHL.
 Waziri wa Biashara na Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Amina Salum Ali, akiongozana na Meneja Mkazi wa DHL Express hapa nchini, Bw. Paul Makolosi, mara baada ya kufungua semina ya mafunzo kwa wajasiriamali wa Zanzibar, kuhusu fursa ya kulifikia soko la Kimataifa kupitia mitandao ya kijamii
 Mhe. Waziri akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa DHL, na wajasiriamali.
 Mhe. Waziri akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa DHL, na wajasiriamali.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages