Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeripoti leo kuwa raia wasiopungua 232 wameuawa huku wanawake na mabinti 120 wakikabwa katika mashambulizi ya vikosi vya serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waitifaki wao.
Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa vikosi vya serikali ya Sudan Kusini na wanamgambo wanaowaunga mkono walitekeleza mauaji hayo ya raia katika vijiji vinavyodhibitiwa na upinzani. Taarifa ya Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa uchunguzi uliofanywa na umoja huo umewataja makamanda watatu wanaoshukiwa kuhusika pakubwa katika machafuko katika jimbo la Unity baina ya Aprili 16 na Mei 24 mwaka huu; machafuko ambayo yanatajwa kuwa ni jinai za kivita. Zeid Ra'ad al Hussein Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa wahusika wa jinai hizo hawapasi kuachwa hivi hivi bila ya kuchukuliwa hatua.
Aidha itakumbukuwa kuwa, makumi ya maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi kufuatia vita vya ndani vilivyoikumba Sudan Kusini mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇