Rais Donald Trump wa Marekani amewataja washauri wake ndani ya White House kuwa ni wapumbavu na kukiri kwamba hitilafu zimeshadidi zaidi ndani ya serikali yake.
Gazeti la New York Times limefichua kuwa, mwezi Machi mwaka huu Donald Trump alifanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin na kujibu malalamiko yake dhidi ya wafanyakazi wa White House ambao alisema wanakwamisha juhudi za kuboresha uhusioano wa nchi hizo na hata wanazuia mawasilino baina ya viongozi hao wawili kwa kusema: Uziwatilie maanani wapumbavu hawa".
Ripoti ya New York Times imeongeza kuwa, wakati Putin alipomwambia Trump kwamba maafisa wa Ikulu ya White House wanatatiza na kuzuia mawasiliano ya simu baina na viongozi hao wawili, Trump alimwambia: "Watu hawa ni wapumbavu na wala usiwasikilize."
Marais wa Marekani na Russia wanatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo Jumanne ijayo katika mji mkuu wa Finland, Helsinki.
Tangu Donald Trump aliposhika hatamu za kuongoza Marekani hitilafu zimeshadidi baina ya maafisa wa White House kwa kadiri kwamba, shirika la habari la Associated Press linasema kiwango cha kubadilishwa wafanyakazi ndani ya Ikulu ya Rais wa Marekani kimetia fora na kuweka rekodi mpya
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇