Lumumba, Dar es Salaam
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Christopher Kajoro Chiza (pichani) kuwa Mgombea wake wa Ubunge katika uchaguzi mdogo utakaofanyika katika Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma, huku kikitaka jitihada za kuongeza tija, ufanisi, faida, utumishi wa watu, uadilifu, vita dhidi ya rushwa na kupambana na ubadhirifu wa mali za Chama na Umma na uchapakazi katika Chama na Serikali ziendelezwe maradufu.
Hayo yamejiri leo katika kikao cha Kamati Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Cahama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao makuu aya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli.
Taarifa iliyotolewa na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, imesema katika kikao hicho pia wajumbe wa Kamati Kuu kwa Kauli moja wamempongeza Rais Dk. John Magufuli, kwa kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwa kasi kubwa ya upelekaji maendeleo na huduma za kijamii hasa katika maeneo ya pembezoni na mijini.
"Kikao cha Kamati Kuu Maalum kimetafakari kwa kina na kuwa na mjadala mpana juu ya Mageuzi Makubwa yanayofanyika katika Chama na Jumuia zake, Serikali na Taasisi zake. Wajumbe kwa pamoja wameridhishwa na kuweka kauli kwamba jitihada hizi za kuongeza tija, ufanisi, faida, utumishi wa watu, uadilifu, vita dhidi ya rushwa na kupambana na ubadhirifu wa mali za Chama na Umma na uchapakazi katika Chama na Serikali ziendelezwe maradufu", imesema taarifa hiyo.
Imesema, pia kikao kimepokea na kupongeza taarifa ya kuwasili kwa ndege kubwa ya Serikali, mpya na ya kisasa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakayokodishwa kwa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL).
Aidha, Kamati Kuu Maalum imempongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake uliojaa hekima na uzalendo wa kuwa na utaratibu wa kukaa pamoja kwa mazungumzo na kupokea maoni na ushauri juu ya masuala ya nchi kwa ujumla na Viongozi wastaafu wa Kitaifa.
Your Ad Spot
Jul 10, 2018
Home
Unlabelled
CCM YATEUA MGOMBEA JIMBO LA BUYUNGU, YANOGEWA NA KASI YA RAIS DK. MAGUFULI NA KUTAKA IONGEZEKE MARADUFU
CCM YATEUA MGOMBEA JIMBO LA BUYUNGU, YANOGEWA NA KASI YA RAIS DK. MAGUFULI NA KUTAKA IONGEZEKE MARADUFU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇