LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 28, 2018

UMOJA WA MATAIFA WALAANI BOMOA BOMOA YA KIBERA, NAIROBI

Operesheni ya kuwahamisha watu kutoka makazi ya Kibera, jijini Nairobi huko nchini Kenya imezusha kelele na lawama kutoka pande mbalimbali ukiwemo Umoja wa Mataifa.
Watalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Kenya isitishe zoezi hilo mara moja. Wataalamu wa kutetea haki za binadamu wa shirika la Umoja wa Mataifa (OHCHR) wamelaani hatua ya kuwatoa maelfu ya watu majumbani mwao kwenye eneo hilo la mabanda la Kibera lililo kusini magharibi mwa jiji la Nairobi.
Watalaamu hao wanaitaka serikali ya Kenya isitishe zoezi hilo mpaka pale utaratibu wa kisheria na usalama wa kutosha utakapofanyika. 
Rais Uhuru Kenyatta ambaye serikali yake inatupiwa lawama kuhusiana na bomoa bomoa ya Kibera
Kulingana na taarifa liyotolewa na ofisi ya kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki za binadamu kwa vyombo vya habari, zoezi hilo lililoanza alfajiri ya tarehe 23 mwezi huu wa Julai litawaathiri zaidi ya wakazi elfu 30 ambao wataachwa bila makazi. Tangu operesheni hiyo ilipoanza takriban watoto 2000 hawaendi shule.
Wanaopinga operesheni hiyo wanasema kuwa, bomoa bomoa hiyo imefanyika kinyume na makubaliano ya hapo awali kati ya Mamlaka ya Barabara za Mijini, Kenya Urban Roads Authority, KURA, Tume ya Kitaifa ya Ardhi na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu Nchini Kenya, KNCHR. Operesheni hiyo ilianzishwa bila ya kutolewa taarifa ya mapema na bila ya kuwepo na mpango wowote wa kuwapatia watu makazi mbadala.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages