LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 27, 2018

MOI TUGHE IMEPATA KATIBU MPYA

 Mwenyekiti wa Tawi la TUGHE MOI Privatus Masula (kulia) akitoa utambulisho meza kuu. kuanzia kulia ni Mdhamini wa TUGHE Taifa na Dokta wa Amana Hospitali, Yonah Mabela na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Ilala Dar es Salaam, Tabu Mambo
 Mdhamini wa Tughe Taifa, Dokt.Yonah Mabela akizungumza jambo kabla ya kuanza uchaguzi wa kumpata Katibu wa Tughe wa Tawi la (MOI)
 Katibu wa TUGHE Mkoa, Tabu Mambo akifafanua jambo kabla ya uchaguzi mdogo wa kuchagua katibu wa tawi la (MOI) na wajumbe 2 wa Tawi hilo
 Sehemu ya wajumbe wa TUGHE MOI wakifuatilia jambo
 Katibu wa TUGHE Mkoa Tabu Mambo akifafanua jambo kabla ya uchaguzi mdogo wa kuchagua katibu wa tawi na wajumbe 2
 Mgombe wa nafasi ya Katibu Musa Migabo akijieleza kwa wanachama na kuomba kura
 Mgombe wa nafasi ya Katibu Norroh  Juma Naseib akijieleza kwa wanachama na kuomba kura
 Mgombe wa nafasi ya Katibu Mkubwa Suleiman akieleza kwa wanachama na kuomba kura
  Katibu wa TUGHE mkoa Tabu Mambo akifafanua jambo kabla ya uchaguzi mdogo wa kuchagua katibu wa tawi na wajumbe 2
 Viongozi wa TUGHE MOI na TUHGE Mkoa pamoja na wawakilishi wa wagombea katika zoezi la kuhesabu kura
 Baadhi ya wajumbe wa TUGHE MOI wakifuatilia uchaguzi kwa umakini
 Baadhi ya wajumbe wa TUGHE MOI wakifuatilia uchaguzi kwa umakini
 Sehemu ya wajumbe wa TUGHE MOI wakiwa wanajaza fomu za uchaguzi
Sehemu ya wajumbe wa TUGHE MOI wakifuatilia jambo
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akimpongeza katibu mteule, Mkubwa Ali Suleiman.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

NA KHAMISI MUSSA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI,  Dkt.  Respicious Boniface amempongeza  kwa kuchaguliwa kuwa Katibu wa TUGHE Tawi la MOI. Bwa, Suleiman  amewabwaga wagombea wenzake wawili kwa kura 55, pia Suleimani alianza kwa kumshukuru Mungu.

 Awali ya yote namshukuru Mungu na uongozi makini wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi yetu,  Dkt Respicious Boniface kwa kuwa pamoja na chama hiki na kushirikiana bega kwa bega na Tawi letu la Tughe MOI pia niwashukuru wanachama wote kwa kuniamini kwa kunipa ushindi wa kimbunga kwa kuwaacha wenzangu wawili kwa kura 55 aliendelea. 

Kwa kushirikiana na wanachama wenzangu ninahitaji kuwaletea mabadiliko makubwa katika chama chetu, katika kuboresha ramani ya Tawi la MOI na wanachama waanze kupata matunda na kuongeza hamasa kwa wanachama ili tuweze kuvuna wanachama wengi.

Mpango mkakati ni kuwajengea uwezo na uwelewa katika kuwapeleka katika semina mbalimbali na mafunzo kwa ujumla ilikuwajengea uwezo ili na wao baadae waweze kuwa viongozi.

Pia njia nyingine nikubuni vyanzo mbalimbali na kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itakayoongeza tija katika kuinua kipato cha chama na kuongeza uhusiano zaidi kati ya chama na mwajiri (uongozi) wa Taasisi kwani bila uongozi hatuwezi kusimama. 

Migogoro mbalimbali nitahakikisha ina pungua kwa kasi kati ya mwajiri na wanachama kwa kutowa elimu namna ya kufanya kazi na kuepusha baadhi ya matatizo ili tuwe tunalifanyia kazi dhumuni la TUGHE ambalo linayutaka  kuboresha maelewano kati ya mwajiri na mwajiriwa (mwana chama) ilikuleta amani sehemu ya kazi.

Kwa kumalizia niseme ambalo ninatarajia katika uongozi wangu ni kuhakikisha kila mwanachama wa TUGHE nikumtegengenezea mazingira ajione mwanachama kutokana na katiba ya TUGHE na vyama vingi husahau kuwatunza wanachama wake na nitapenda kujua mapungufu ili kupata kuzitatua nikishirikiana na wenzangu.

Ili wanachama waweze kukaa sehemu moja na niweze kuvuna wanacha wengi zaidi ili kuongeza namba ili wakisha fika wahisi kuwa wamefika na kuweka mipango katika mazingira yanayokubalika.

Na Mawenyekiti wa Tawi hilo la MOI, Privatus Masula alisema, 
Ninashukuru uchaguzi umekwenda vizuri pia nina shukuru meza kuu kwa kusimamia vizuri uchaguzi huo,ambapo uchaguzi huu umefanyika Novemba 26 ni kuziba nafasi ya aliyekuwa katibu wa Tawi hilo

 Ambaye liyekaa katika kipindi cha miaka kumi lakini amekiuka taratubu za uongozi, kuvunja sheria za uongozi, kwahiyo tulikaa kikao cha Halmashauri na kushauriana na kuona amekwenda kinyume na taratibu na Katiba ya TUGHE.

Kwa hiyo tukamuomba ajiuzuru katika kulinda chama na kuendeleza soldalite ya sehemu ya kazi kwa hiyo amejiuzuru na kuweza kufanya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages