LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2018

JUA SAHEL AFRIKA KUZALISHA ASILIMIA 70 YA MAHITAJI YA UMEME DUNIANI

Ukanda wa Sahel barani Afrika umeelezwa kuwa mbioni kujikomboa na changamoto ya nishati kuanzia mijini hadi vijijini.
Hii ni kutokana na mpango mpya wa Umoja wa Mataifa ambao lengo ni kutumia rasilimali kubwa ya asili ukanda huo ambayo ni jua, kuzalisha umeme kwa matumizi ya majumbani na shughuli zingine, sio tu Sahel peke yake bali Afrika nzima na zaidi.
Takriban asilimia 70 ya mahitaji ya umeme duniani yanaweza kutolewa kwa kuvuna nishati ya jua kali liwakalo Ukanda wa Sahel barani Afrika. 
Hayo ni kwa mujibu wa mpango mpya wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya ukanda wa Sahel uliozinduliwa hivi karibuni kwa lengo la kuchapuza ushirikiano wa mafanikio na amani ya kudumu kwa nchi 10 zinazounda Ukanda huo.
Rachel Kyte, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nishati endelevu kwa wote
Rachel Kyte, ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nishati endelevu kwa wote , anaamini kwamba Sahel iko katika mabadiliko ambayo nishati ya jua inaweza kuzalisha umeme katika ukanda huo na hata kwa jamii za nje ya ukanda huo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa hususan Shirika la Chakula na Kilimo la Duniani (FAO), Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) na baadhi ya taasisi zisizo za kiserikali zzimeendelea kutoa indhari kuhusiana na uhaba wa chakkula katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages