Wizara ya Madini imekabidhi eneo la ujenzi wa Kituo cha Umahiri wilayani Songea Mkoani Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) wa Ujenzi wa Kituo cha Umahiri wenye lengo la kusaidia kuwaongezea ujuzi wachimbaji wadogo kwa kutiliana saini za ujenzi na Mkandarasi wa vituo hivyo kampuni ya SUMA JKT na kampuni ya Y&P akiongea wakati wa Makabidhiano hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mkurugenzi wa Sheria Kutoka Wizara hiyo Bw. Edwin Igenge amemtaka Mshauri elekezi wa Mradi huo kampuni ya Y&P kumsimamia mkandarasi ambayo nikampuni ya SUMA JKT bila hofu ili kuhakikisha wanafanya kazi katika viwango vilivyokubaliwa na ambavyo vipo kwenye mkataba.“Tunawakabidhi mkataba huu muanze kufanya kazi kama ilivyokubaliwa, nanakuagiza mshauri elekezi uhakikishe unamsimamia mkandarasi bila woga,dhumuni ni kuhakikisha anafanya kazi yenye ubora kulingana na mikatabatuliyoisaini leo”. Alisema Bw. IgengeAkiongea wakati akimkabidhi mchoro wa mradi huo, Msanifu Majengo kutokaKampuni ya Y&P Bw. Benjamin Kasiga amemtaka mkandarasi kufanya kazi kamaalivyoelekezwa katika mkataba na kwa kuzingatia viwango vinavyojitajika nchini.Naye Muwakilishi kutoka kampuni ya SUMA JKT Mhandisi Joseph Jeremiah amehidikutekeleza kulingana na maelekezo yaliyoainishwa kwenye michoro na kufanya kazikwa ubora wa hali ya juu.Hatua hii ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni na Waziri wa Madini Mhe.Angelah Kairuki wakati akiwasilisha Bungeni Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ambapo alieleza kuwa mradi huu utatekelezwa katika maeneo ya Mpanda, Songea, Chunya, Tanga, bariadi, Bukoba na Musoma pamoja na upanuzi wa miundombinu ya Chuo Cha Madini Dodoma kwaajili ya kuwezesha utekelezaji wa shughuli za madini zinazotekelezwa na ChamaCha Wachimbaji Madini Wanawake
Your Ad Spot
Jul 16, 2018
Home
Unlabelled
WIZARA YA MADINI YAMTAKA MSHAURI ELELEKEZI MRADI WA SMMRP KUTOMUHOFIA MKANDARASI
WIZARA YA MADINI YAMTAKA MSHAURI ELELEKEZI MRADI WA SMMRP KUTOMUHOFIA MKANDARASI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇