Shirikisho la soka Nchini (TFF) limetakiwa kigezo za umri wa wachezaji wanaowandaa kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 17 (U17) ili kuepuka kuvunja sheria.
Hayo yamesemwa na Leodegar Tenga wakati wa uiznduzi wa Kamati ya maandalizi ya Michuano hiyo, ambapo ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Akizindua Kamati hiyo yenye wajumbe 25 kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika nchini mwaka 2019, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe alisema wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo atakuwa yeye, Makamu Mwenyekiti ni Tenga ambaye Mjumbe wa CAF na Rais wa heshima wa TFF na Hendry Tandau kutoka Kamati ya Olimpiki nchini ambaye atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kamati.
Kamati hiyo inao wajumbe mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkurugenzi wa ATCL Ladislaus Matindi na Mohamed Dewji.
Mwakyembe amewapongeza wajumbe walioteuliwa na kusema kuwa uteuzi wa wajumbe hao wa kamati ulizingatia sekta muhimu zitakazo husika moja kwa moja katika kufanikisha mashindano hayo.
“Nawapongeza wajumbe wote kwa kukubali uteuzi huu maana kazi ya kamati hii si ya kulipwa bali ni kujitolea kwa manufaa ya nchi yetu na ninaimani kubwa kuwa tutafanya kazi nzuri na kwa kufanikisha mashindano haya tutakuwa tumelipa taifa heshima kubwa katika ulimwengu wa soka”, alisema Mwakyembe.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇