Tuesday, July 10, 2018

UN: VIKOSI VYA SERIKALI YA SUDAN KUSINI NA WAITIFAKI WAKE VIMEUWA MAMIA YA RAIA

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeripoti leo kuwa raia wasiopungua 232 wameuawa huku wanawake na mabinti 120 wakikabwa katika mashambulizi ya vikosi vya serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waitifaki wao.
Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa vikosi vya serikali ya Sudan Kusini na wanamgambo wanaowaunga mkono walitekeleza mauaji hayo ya raia katika vijiji vinavyodhibitiwa na upinzani. Taarifa ya Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa uchunguzi uliofanywa na umoja huo umewataja makamanda watatu wanaoshukiwa kuhusika pakubwa katika machafuko katika jimbo la Unity baina ya Aprili 16 na Mei 24 mwaka huu; machafuko ambayo yanatajwa kuwa ni jinai za kivita. Zeid Ra'ad al Hussein Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa wahusika wa jinai hizo hawapasi kuachwa hivi hivi bila ya kuchukuliwa hatua.
Zeid Ra'ad al Hussein, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN 
Aidha itakumbukuwa kuwa, makumi ya maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi kufuatia vita vya ndani vilivyoikumba  Sudan Kusini mwaka 2013.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Mdau, andikamaoni yako hapa yasaidie kujua wewe unafikiri nini kuhusu posti hii. Tafdhali, Maoni yako yasiwe ya uchochezi wa aina yoyote.. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

CCM Blog. Powered by Blogger.