LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 2, 2015

NAPE AENDELEA NA ZIARA KATIKA VYOMBO VYA HABARI ATEMBELEA GAZETI LA RAIA TANZANIA LEO



 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa gazeti la Raia Tanzania na Raia Mwema katia ofisi za magazeti hayo jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa kikao na wahariri wa magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akizungumza huku Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akimsikiliza kwa makini.
Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa kampuni ya Magazeti ya Raia Mwema.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Raia Mwema Ndugu Mbaraka Islam pamoja na Meneja wa Matangazo wa kampuni ya Raia Mwema Ndugu John Daniel wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye.


KATIBU wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo ametembelea ofisi za kampuni ya Raia Mwema inayotengeneza magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania, kwa lengo la kushukuru na kueleza mikakati ya chama chake
.

Itakumbukwa miezi kadhaa iliyopita kabla ya uchaguzi mkuu Nape, alitembelea vyumba vya habari akianzia na Raia Mwema kueleza pamoja na mambo mengine namna walivyojipanga na uchaguzi ikiwemo kupata mgombea urais.

Akizungumza jana katika ofisi hizo alipokutana na wahariri pamoja na viongozi mbalimbali wa kampuni hiyo alisema, wanafurahishwa na kasi ya Rais John Magufuli, kwa sababu kinachotendeka sasa walikipanga hata kabla ya uchaguzi.

“Tulitaka mtu wa aina hii, haya mabadiliko tuliyarataji hivyo hatushituki kuyaona, tunachotaka kuwaambia wananchi tu ni kuwa baada ya kumaliza serikalini mabadiliko yatahamia kwenye chama,” alisema Nape.  



BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages