LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 22, 2026

UJUMBE WA MKOA WA DAR ES SALAAM ULIOPO QATAR WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI HUMO

CCM Blog, Qatar

Ujumbe wa viongozi na wataalamu kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, umetembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na kukutana na Balozi wa Tanzania nchini humo.


Katika mazungumzo, ujumbe umepata maelezo kuhusu shughuli za Ubalozi, maandalizi ya timu ya vijana ya Tanzania, Serengeti Boys, kwa mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA la vijana chini ya miaka 17, pamoja na ratiba ya ziara katika maeneo mbalimbali iliyoandaliwa na Ubalozi.


Ujumbe huo unajumuisha Katibu Tawala wa Mkoa, Makatibu Tawala wa Wilaya na wataalamu kutoka Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.


Lengo la ziara ni kujifunza uzoefu wa Qatar katika kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa, ikiwemo Kombe la Dunia la FIFA 2022, ili kusaidia kuboresha maandalizi ya AFCON 2027 nchini Tanzania.






No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages