Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Stanley Mkandawire (MNEC) leo Novemba 13, 2026, ameongoza Sekretarieti ya CCM ya Mkoa na Makatibu wa CCM wa Wilaya za mkoa kumpokea Katibu wa CCM Wilaya ya Magu Frata Andrea Katumwa ambae amefiwa na mtoto wa wake.
Baada ya mapokezi hayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere International Airport, Katibu Mkandawire aliongoza waombolezaji kwenda msibani, nyumbani kwa Katibu Frata Andrea Katumwa, Pugu Kinyamwezi ambako, ambako taratibu zingine za maziko zinafanyika.
Katibu Mkandawire aliongozana na Sekretarieti ya CCM ya Mkoa wa Dar es Salaam, Katibu wa CCM wilaya ya Ilala na Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo
Akizungumza nyumbani kwa katibu Frata, Katibu Mkandawire ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki huku akisema kwa niaba ya chama anaendelea kuwaombea katika kipindi hiki kigumu na kwamba CCM mkoa kwa kushirikiana na Makatibu wa CCM wa wilaya wameahidi kushirikiana kusafirisha kwa ndege mwili wa marehemu pamoja na mama mzazi.
Mwili wa marehe unatarajiwa kusafirishwa Jumapili, Novemba 15, 2026 kwenda wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya maziko.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Stanley Mkandawire (MNEC) akisaidiana na waombolezaji kumsaidia Katibu wa CCM Wilaya ya Magu Frata Andrea Katumwa.







No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇