LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2026

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI ATEMBELEA OFISI YA DC ARUMERU, KUJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI


Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Marianne Young, amemtembelea Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Neema Lugangira, ofisini kwake, ambapo viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Wilaya ya Arumeru na Serikali ya Uingereza, hususan katika kuvutia uwekezaji na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa wawekezaji.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo wilayani Arumeru pamoja na umuhimu wa kuweka mazingira wezeshi yatakayowavutia wawekezaji wapya kutoka Uingereza na kuwawezesha wawekezaji waliopo kuendeleza shughuli zao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Neema Lugangira, amekubaliana na Balozi Marianne Young kuwa mara baada ya kukamilisha ziara yake ya Kata kwa Kata wilayani humo, atawasilisha vipaumbele vya maendeleo ya Wilaya ya Arumeru ili kubainisha maeneo mahsusi ya ushirikiano kati ya ofisi yake na Ubalozi wa Uingereza.

Hatua hiyo inalenga kuweka msingi wa ushirikiano utakaosaidia kutambua fursa za uwekezaji na kuhamasisha utekelezaji wa miradi itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Arumeru.

#ArumeruKimataifa
#MaendeleoArumeru #KataKwaKata
#TukutaneSite




 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages