LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2026

ASKOFU CHANDE AWATAKA WANASIASA KUACHA CHUKI, WAJIFUNZE KUPITIA DABI YA SIMBA NA YANGA

ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assemblies of God Tanzania (KAG), Dkt. Evance Chande, amewataka wanasiasa kuacha chuki bali kinachotakiwa ni kujifunza kupitia Dabi ya watani wa jadi Yanga na Simba ambayo daima wakishindana huishia kutaniana badala ya kupigana au kuzua magomvi.

Aidha amewataka watanzania kukataa migawanyiko na kuwa makini dhidi ya watu wanaochochea mifarakano, akisisitiza kuwa kukubali hali hiyo kunaweza kuhatarisha umoja, amani na utulivu wa nchi. Akizungumza Novemba 8, 2026, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kanisa la KAG, eneo la Lugala, Nala jijini Dodoma, Askofu Chande alisema wananchi wana wajibu wa kulinda umoja wa taifa kwa kutoruhusu tofauti mbalimbali kutumiwa kuwagawanya. Alisisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kuwa sehemu ya kuimarisha mshikamano badala ya kuunga mkono vitendo vinavyoweza kuleta mifarakano katika jamii. Kupitia harambee hiyo, jumla ya Sh milioni sita zilichangwa papo kwa papo, huku washiriki wengine wakitoa ahadi za kuchangia fedha kwa ajili ya kufanikisha hatua hiyo ya ujenzi. Ujenzi wa kanisa hilo kubwa umefikia hatua ya linta, hatua inayotangulia kuendelea na kazi nyingine za ujenzi kuelekea kukamilika kwa jengo hilo. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini kutoka madhehebu tofauti, waliotoka ndani ya Dodoma na mikoa mingine, ikiwa ni sehemu ya kushiriki tukio hilo la uwekaji wa jiwe la msingi.



 ASKOFU Mkuu wa Makanisa ya Karmeli Assemblies of God Tanzania (KAG), Dkt. Evance Chande

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages