LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 28, 2026

CHACHA ATAJA SIFA ZA NDILITO, AWASIHI WANANCHI KUMPA KURA.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Idara ya Organaizesheni, Paul Chacha, amemtaja mgombea wa chama hicho katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Chamwino, Dkt. Netho Ndilito, kuwa kada mwaminifu, msomi na mzalendo aliyeiva ndani ya chama hivyo kuwaomba wananchi kumpa kura.


Chacha ametoa kauli hiyo Oktoba 28, 2026, wakati akiwa Mgeni Rasmi katika Mkutano wa Hadhara wa Kumnadi Dkt. Ndilito, ambapo amewataka wanachama wa CCM kushikamana katika kumnadi mgombea huyo na wananchi wa Chamwino kumpa kura ili aendelee kutekeleza Ilani ya CCM.

Amesema CCM ni chama imara chenye misingi ya umoja na mshikamano, huku akiipongeza Kamati ya Siasa ya Mkoa na Wilaya ya Chamwino kwa maandalizi mazuri ya mkutano huo.

Aidha,  amewasisitiza wananchi wa Jimbo la Chamwino kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Novemba 4, 2026, wakizingatia amani na utulivu.

Dkt. Ndilito aliteuliwa na Kamati Kuu ya CCM katika kikao chake kilichofanyika Oktoba 11, 2026, Kizimkazi, Zanzibar, kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mdogo unaofanyika kufuatia uteuzi wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Deogratius John Ndejembi, kuwa Makamu wa Rais.






 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages