LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 17, 2026

CDE MKANDAWIRE AFUNGUA SEMINA YA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA KATA NA MATAWI, KATA YA TANDALE

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam ndugu Stanley Mkandawire (MNEC) leo tarehe 17 Oktoba 2026, Tandale amefungua Mafunzo ya viongozi wa Kata na Matawi katika Kata ya Tandale.


Katibu Mkandawire amefungua mafunzo hayo ikiwa ni muendelezo wa mafunzo ya viongozi yanayoendelea kutolewa katika Mkoa yakilenga kuwajengea uwezo viongozi wa CCM huku mada mbalimbali zikifundishwa.


Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Katibu Mkandawire amesisitiza Umuhimu wa viongozi kukijua Chama ikiwemo Itikadi na misingi yake pia amesisitiza zaidi kwa viongozi kuyatumia mafunzo hayo kuongeza wanachama wapya na kulipa Ada za wanachama kwa wakati.


Katika hatua nyingine, Katibu Mkandawire amewaomba viongozi hao kuendelea kumsemea mema Mwenyekiti wa CCM Rais  Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika Mkoa wa Dar es Salaam 


"Miaka kadhaa iliyopita, kutoka Tandale kwa Tumbo hadi kwenye Ofisi za Kata palikuwa hapapitiki kwa sababu ya ubovu wa Barabara.


Lakini pia kulikuwa na soko ambalo sio la kisasa na hata zahanati iliyokuwepo sasa serikali imetenga bajeti kuanzia mwezi ujao inaenda kuboresha kuwa kituo cha Afya cha ghorofa tano lakini pia  Sasa Serikali imechukua hatua ya kujenga Barabara nzuri na Soko la kisasa", amesema Mkandawire


Ametoa onyo kwa viongozi ambao hawatashiriki mafunzo hayo yanayoendelea kutolewa katika Mkoa wa Dar es salaam, kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kutorudishwa majina yao watakapogombea  kwenye Uchaguzi wa Mwakani 2027.



KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages