LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 7, 2026

ZAIDI YA WAHITIMU 62,000 TIA WAINGIA SOKO LA AJIRA, UJASIRIAMALI

JUMLA  ya wanafunzi 62,680 wamehitimu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwa mwaka 2025/2026 na kuingia katika soko la ajira, ujasiriamali na kutoa huduma mbalimbali za kitaaluma

Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo alisema mafanikio ya TIA hayapimwi kwa ongezeko la idadi ya wanafunzi na kampasi pekee, bali pia kwa idadi ya wataalamu wanaozalishwa na kuingia katika soko la ajira.

‎.Alisema takwimu hizo zinaonesha mchango wa TIA katika kuzalisha rasilimali watu yenye ujuzi unaohitajika katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na maendeleo ya Taifa.

‎“Ukuaji wa TIA haujikiti tu katika idadi ya wanafunzi, bali unaendelea kutengeneza rasilimali watu inayohitajika katika uchumi wa Taifa letu,” alisema.

Alisema katika mwaka wa fedha 2026/27, TIA itaendelea kuimarisha programu za elimu, kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya juu na kuwekeza katika mazingira bora ya kujifunzia ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya elimu ya uhasibu, biashara, uchumi na maeneo mengine yanayohusiana na taaluma hizo.

Prof. Pallangyo alikuwa akielezea utekelezaji wa TIA katika mwaka wa fedha 2025/26 pamoja na mwelekeo wa taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari–MAELEZO, jijini Dodoma.


 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages