Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika amezidi kuibana Serikali bungeni Dodoma Septemba 4, 2026 kwamba inachukua hatua gani za haraka kuwaondolea Wananchi kero inayotokana na kutumia barabara ya Makambako – Songea ambayo imechakaa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, Godfrey Kasekenya amejibu akama ifuatavyo;
Mheshimiwa Spika, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Makambako – Songea (km 295) umekamilika. Ukarabati wa barabara hii unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo kwa sasa kazi zinaendelea kwa sehemu ya Songea – Lutukira (km 95). Kwa sehemu zilizobaki za Lutukira – Lwangu (km 100) na Lwangu – Makambako (km 100), Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇