LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 19, 2026

JKT WATILIA MKAZO MAFUNZO YA UZALENDO KIDIJITALI


 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema somo la Uzalendo na Uzalendo wa Kidijitali kwenye silabasi za mafunzo ya JKT litaendelea kuboreshwa zaidi ili kuelimisha vijana umuhimu wa kutumia vema mitandao ya kijamii.

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo leo Septemba 18, 2026 wakati akifunga ukurasa wa zoezi la uhitimishaji wa mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Linda Amani na Kujitolea Operesheni Nishati Safi katika Kikosi cha Kanembwa JKT kilichopo mkoani Kigoma.

Akiwasilisha salamu za Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Brigedia Jenerali Lawrence Lugenge amewapongeza vijana hao kwa kukubali kujiunga na mafunzo ya JKT na kuwataka kuendeleza yale yote waliyojifunza.

Akitoa taarifa mafunzo kwa ujumla Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT Brigedia Jenerali Peter Mnyani amewapongeza vijana hao kwa kuwa watiifu katika kipindi chote cha mafunzo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar Kanali Makame Daima amewaasa vijana wahitimu kuendelea kuulinda Muungano wa Tanzania.

Akitoa taarifa fupi ya mafunzo mbele ya mgeni rasmi, Kamanda Kikosi Kanembwa JKT Kanali Mantage Nkombe amesema Vijana wote waliohitimu mafunzo yao wamejifunza kwa nadharia na vitendo kwa kuzingatia silabi ya mafunzo husika na wamefaulu kwa viwango vinavyokubalika ndani ya JKT.

Zoezi la ufungaji wa mafunzo ya JKT lilianza rasmi Septemba 8, 2026 katika vikosi vyote vya mafunzo vya JKT na kwa mara kwanza mafunzo hayo yamefanyika kwa kujumuisha makundi mawili ambayo ni Kundi kundi la Kujitolea Operesheni Nishati Safi na kundi la Lazima (Mujibu wa Sheria).


 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages