LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 12, 2026

DC MPOGOLO AWAAGIZA HALMASHAURI, TARURA NA DAWASA KUZIBUA MITARO KARIAKOO

CCM Blog, Kariakoo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mh. Edward Mpogolo, ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuanza mara moja kuzibua mitaro, mifereji na chemba za kupitisha maji taka maeneo ya Kariakoo.

Ametoa agizo hilo alishirikiana na viongozi na wananchi kufanya usafi leo Jumamosi, Septemba 12, 2026, ikiwa ni utekelezaji wa kampeni endelevu ya usafi inayofanyika kila Jumamosi.

Ufanyaji usafi huo ulioongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Abdul Muhite, akishirikiana na Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa na Wilaya.

Viongozi wengine walioshiriki ni pamoja Diwani wa Kariakoo Haji Manara, Diwani wa Jangwani  Mohamed Zaidi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Charangwa Selemani,
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuru Mabelya na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo.

Wengine ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Rajabu Amiry, akiwa ameambatana na wasanii wa filamu Tanzania, pamoja na Kampuni za Usafi za SATEK, KAJENJERE, TIRIMA na WEJISA, Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK) na KAWASSO.

Mhe. Mpogolo amesema mitaro na mifereji iliyoziba kutokana na taka inaweza kusababisha maji kushindwa kupita wakati wa mvua na hivyo kuhatarisha usalama wa wananchi, biashara na miundombinu.

“Natoa agizo kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, TARURA na DAWASA, kuanza mara moja kazi ya kuzibua mitaro, mifereji na chemba za maji pamoja na kuondoa takataka zilizoziba mifereji hiyo. Takataka hizi zinasababisha mifereji kushindwa kufanya kazi ipasavyo hivyo kuweza kusababisha madhara makubwa wakati wa mvua.” amesema Mh. Mpogolo.

Amesema Mamlaka za hali ya hewa zimeendelea kutoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa, hivyo ni muhimu maandalizi yakafanyika mapema kwa kuhakikisha mitaro na mifereji inakuwa wazi na inafanya kazi ipasavyo.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Rdward Mpogolo akkitoa agizo hilo.




 








No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages