Katibu wa Chana Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Stanley Mkandawire na Katibu
wa CCM Mkoa wa Mwanza Cde Omar Mtua, juzi walifika kutoa salamu za pole
kwa Mwenyekiti wa CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha
mwenza wake Marehemu Hafidh Ameir Hassan.
Cde Mkandawire na Cde Mtua wametia salamu hizo kwa niaba ya Makatibu wa CCM wa Mikoa yote ya Tanzania.
Wakiwasilisha
salam hizo, wameeleza masikitiko yao na kumuombea Mwenyekiti Dk. Samia
na familia ndugu na marafiki Mungu awape nyoyo za subra katika kipindi
hiki kigumu cha maombolezo.
“Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape
subra, nguvu na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
Mwenyezi Mungu amsamehe marehemu Hafidh Ameir Hassan, amrehemu na amlaze
mahali pema peponi. Amina.”
INNA LILLAHI WA INNA ILAYHI RAJI’UN
Katibu wa Chana Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Stanley Mkandawire na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Cde Omar Mtua (Kulia), wakitoa salamu za pole juzi, kwa Mwenyekiti wa CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mwenza wake Marehemu Hafidh Ameir Hassan.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇