LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2026

WANAMUZIKI WAMSHUKURU DKT. MDAKU KWA KUWAPIGA TAFU

 Ndoto za vijana kutoka Jimbo la Malinyi za kupata elimu ya ufundi na kujijengea maisha bora zimeanza kutimia baada ya kuripoti rasmi katika Chuo cha Victory kilichopo Morogoro kwa ajili ya kuanza masomo yao, wakieleza kuwa fursa hiyo imepatikana kupitia jitihada za Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku.


Wakizungumza mara baada ya kuwasili chuoni hapo, wanafunzi hao  wamesema kuwa wamepata matumaini mapya ya maisha kupitia fursa ya elimu itakayowawezesha kupata ujuzi, kujiajiri na kushindana katika soko la ajira.


Wameongeza kuwa, kabla ya fursa hiyo walikuwa hawana uhakika wa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali, lakini kupitia maono na juhudi za Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku, sasa wameanza safari mpya yenye matumaini makubwa ya mafanikio.


"Tunamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kutuamini na kutupa nafasi hii. Tumeahidi kusoma kwa bidii ili kurejea Malinyi tukiwa wataalamu watakaoshiriki kuleta maendeleo katika jamii yetu," alisema mmoja wa wanafunzi hao.Kwa upande wake, Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku ameendelea kusisitiza kuwa uwekezaji katika elimu na ujuzi kwa vijana ni msingi wa kujenga taifa lenye nguvu kiuchumi, akiamini kuwa vijana wa Malinyi wakipata fursa sahihi watakuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya jimbo na Taifa kwa ujumla.


Hatua hiyo ni sehemu ya dhamira yake ya kuendelea kuwawezesha vijana wa Malinyi kwa kuwafungulia milango ya elimu, mafunzo ya ufundi na fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi, ili wawe wazalishaji wa ajira badala ya watafuta ajira.




No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages