LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 30, 2026

NMB YAHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KUKUZA BIASHARA

 Benki ya NMB imewataka wafanyabiashara wa Mwanza, Mara na Geita kutumia malipo ya kidijitali na akaunti mahsusi za biashara ili kufikia masoko mapya na kusimamia fedha zao kwa usahihi.


Akizungumza katika jukwaa la NMB Business Executive Network jijini Mwanza, Mkuu wa Idara ya Biashara wa NMB, Deogratius Shirima, alisema mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya wateja yanawalazimu wafanyabiashara kubadili namna wanavyopokea malipo na kuendesha shughuli zao.

Shirima alisema suluhisho za malipo ya mtandaoni za NMB pamoja na NMB SME World Business Credit Card zinalenga kurahisisha miamala ya ndani na nje ya nchi. Pia alisema NMB imeboresha huduma za Bank Guarantee, ambapo dhamana za zabuni zisizohitaji dhamana ya mali (Unsecured Bid Bonds) zinaweza kufikia hadi dola milioni 10 za Marekani bila kuweka dhamana ya mali.

Kwa upande wake Leah Mwakang’ata, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Biashara kwa Wateja Wadogo na wa Kati (SME) wa NMB, aliwahimiza wafanyabiashara kutenganisha fedha binafsi na fedha za biashara kupitia akaunti rasmi. Alisema hatua hiyo inawasaidia wafanyabiashara kufuatilia mapato na matumizi kwa usahihi, kujenga historia nzuri ya kifedha na kupata huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji ya biashara zao.

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Gabriel Mugini, alisema mazingira ya biashara mkoani humo yanaendelea kuvutia wawekezaji. Aliwataka wafanyabiashara kutumia fursa za kifedha na kiteknolojia zinazopatikana ili kupanua shughuli zao.







No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages