LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 1, 2026

MAGANYA ARIDHISHWA NA RUWASA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI KIBITI

Mwenyekiti wa  Jumuiya ya W

azazi Taifa Ndg. Fadhili Maganya  ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji unatekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kibiti.


 Amesema mradi huo ni mkombozi mkubwa katika kuwahudumia  kwa kiasi kikubwa wananchi  na kwamba upatikanaji wa maji safi na salama utawapunguzia adha wanannchi  kwa kutembea umbali mrefu.

Hayo ameyabainisha wakati wa ziara yake ya  kikazi katika Wilaya ya Kibiti yenye lengo la kuweza kuimarisha chama, kuangalia utekelezaji wa Ilani  pamoja na jumuiya zake zote  sambamba na  kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo, ikiwemo  sekta ya elimu pamoja na sekta ya maji.

Mwenyekiti huyo amesisitiza kwa  uongozi wa Ruwasa kuendelea kuhakikisha wanaweka ulinzi wa kutosha katika mradi huo ambapo amesema chanzo hicho ni muhimu sana kwani ndio tegemezi kubwa la wananchi wa Wilaya ya Kibiti katika suala zima la upatikanaji wa maji safi na salama na kuwahimiza kutunza  chanzo cha maji hayo pamoja miundombinu iliyopo.

"Nipende kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati uongozi mzima wa Ruwasa kwa kutekeleza mradi huo wa maji ambao utakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Wilaya ya Kibiti,"amebainisha Mwenyekiti.

Akizungumza katika mkutano wa ndani na wanachama wa chama hicho amewaomba viongozi kuhakikisha  kwamba wanatekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwemo suala la kusimamia fursa za mikopo ya asilimia 10 ambayo inatolewa na Halmashauri.

Pia amewaagiza viongozi wa chama pamoja na madiwani kuhakikisha wanasimamia fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 

Meneja huyo amebainisha kwamba  lengo kubwa la ukarabati wa mradi huo  ni kwa  ajili ya kuweza kutatua changamoto   ya maji ambazo  zinawakabiliwa wananchi wa Wilaya ya Kibiti na kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha ina mtua mama ndoo kichwani
.
Amebainisha  ukarabati wa.mradi wa  maji Kibiti mjini umetekelezwa kwa kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni 312 ambazo fedha hizo zimetolewa  na serikali kuu kupitia mfuko wa maji wa fedha Kitaifa (NWF) na kwamba utakuwa ni  mkombozi mkubwa katika kutatua changamoto hizo zilizokuwa zinawakabili wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa  wazazi Taifa kwa  kutekeleza ilani ys chama kwa vitendo ikiwemo suala la kufanya ziara ya kikazi ambayo imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuweza kukutana na viongozi wa serikali, taasisi wezeshi  pamoja na chama.

Kanali Kolombo amebainisha kwamba hali ya amani na utulivu katika Wilaya ya Kibiti inaendelea vizuri na kwamba katika utekelezaji wa ilani wameweza kupokea kiasi cha  shilingi milioni 528  kwa ajili ya ujenzi  wa shule  ya Mchukwi ambapo pia wamepokeai kisi cghha shilingi milioni 700 kwa lengo la kuboresha miundombinu ya barabara hususan zinazowenda maeneo ya Delta na sehemu nyingine.  
 
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa  ameendelea na   ziara yake  ya kikazi katika Wilaya ya Kibiti ambapo ameweza kupata fursa ya kuzungumza na wanachama wa CCM, viongozi wa serikali,taasisi wezeshi  pamoja na kutembelea baadhi ya  miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta ya maji pamoja na  elimu.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages