LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 21, 2026

ACHENI KUPUUZA MAAGIZO, HOJA ZA KAMATI ZA BUNGE - ADO SHAIBU

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Ado Shaibu, amezionya Halmashauri za wilaya nchini kuacha tabia ya kudharau na kupuuza hoja na maelekezo ya kamati hiyo na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari baada ya kamati hiyo kufanya kikao na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Same jijini Dodoma Agosti 20, 2026.

Akisoma tamko la kamati amewataka viongozi hao kutekeleza maagizo yote ya CAG na yale yanayotolewa na Kamati yake. Hadi jana Agosti 20 kamati hiyo imehoji halmashauri 36 bado 3 watakazomalizia leo Agosti 21. Kwa upande wa Halmashauri ya Same amewarudisha kwenda kutekeleza na wataitwa tena kujiridhisha kama maagizo hayo yote yametekelezwa kama kamati hiyo ilivyoagiza.
"Ifahamike kwamba kamati yake inafanya kazi kwa niaba ya bunge, kuidharau kamati hiyo ni swa na kulidharau bunge kitu ambacho hakikubaliki hata kidogo,"amesema Shaibu.



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Ado Shaibu akizungumza na vyombo vya habari katika kikao hicho.

Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika kikao hicho.







Mmoja wa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same akijibu hoja.


 

https://youtu.be/F0h0FaJ9a1s

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages