LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 19, 2026

NSSF YAVUNA WAJASIRIAMALI SEMINA YA JUKWAA HURU LA WAHARIRI MOROGORO

 Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imevuna wateja wengi baada ya kunadi huduma zake katika semina ya siku tatu ya mafunzo ya ujasiriamali ya "Jifunde kwa Mama Ujasiiamali" iliyoandaliwa na Jukwaa Huru la Wahariri Tanzania (JUWATA) kwa ushirikiano na Mamo Enterpreneurship iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la JKT la Umwema Morogoro Mjini.

Semina hiyo iliyohudhiriwa na zaidi ya wajasiramali 1000 ilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima aliyewakilishwa na Beatrice Njawa, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Julai 13, 2026. Uongozi wa Jukwaa hilo jipya unaoongozwa na Mwenyekiti Richard Mwaikenda na Katibu Mkuu Ahmad Mohamed ulitumia semina hiyo kulitambulisha Jukwaa hilo lililoanzishwa hivi karibuni.


Wajasiriamali wakijisajili kuinga na NSSF wakati wa semina hiyo.

Wajasiriamali wakiwa katika mafunzo.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages