Na CCM Blog, Kunduchi
![]() |
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Cde Stanley Mkandawire, amewaagiza viongozi wa Halmashuri Kuu za Chama katika Matawi ya CCM Kata ya Kunduchi Wilaya ya Kinondoni, kuzingatia ufanyikaji wa vikao kwenye mashina na matawi kwa kufuata taratibu na Katiba ya Chama.
Pia amewataka kuhakikisha maamuzi yote yanayohusu Chama yafanyike kwenye vikao na sio mtu mmoja au watu wawili kwa kuwa kufanya hivyo ni kukihujumu.
Cde Mkandawire ametoa maagizo hayo, jana, Julai 15, 2026, wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na viongozi wa Halmashuri Kuu za Chama katika Matawi ya Mtongani na Tandale Kibaoni, Kata ya Kunduchi Wilaya ya Kinondoni.
”Nawaombeni sana mzingatie sana ufanyikaji wa vikao kwenye mashina na matawi yenu uwe wa kufuata Katiba ya CCM, na maamuzi yote yafanyike kwenye vikao na sio mtu mmoja au watu wawili, kwani kufanya hivyo tutakuwa tunakihujumu Chama", amesema Cde Mkandawire
Katika mikutano hiyo iliyofanyika Ofisi ya CCM tawi la Tandale Kibaoni na mwingine katika ukumbi wa CCM tawi la Mtongani, Cde Mkandawire aliambatana Sekretarieti ya CCM mkoa, lengo likiwa kuwakumbusha viongozi umuhimu wa vikao kwenye mashina yao kwa mjibu wa Katiba.
Pia kuwakumbusha kuhusu kanuni na miongozo ya Chama, Ulinzi wa mali za Chama katika maeneo yao na kubuni miradi ili kukiimarisha Chama kiuchumi.
Cde Mkandawire na Sekretarieti hiyo pia waliitumia mikutano hiyo kuonya makada walionza kampeni mapema za Uchaguzi wa 2027 ndani ya Chama.
Sekretarieti hiyo ya mkoa imeonya na kuelekeza kuwa muda wa kampeni za Uchaguzi wa mwakani ndani ya chama bado, hivyo walioanza kutengeneza makundi na kukigawa chama watachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa katiba na miongozo ya CCM.
Viongozi waliombatana na Cde Mkandawire katika ziara hiyo walikuwa, Haji Kilimo ambae ni Katibu wa Wazazi Mkoa, Hussein Egobano Katibu wa UVCCM Mkoa na Katibu wa UWT Mkoa Sawia Severine, pamoja na Sekretarieti ya CCM wilaya ya kinondoni na Maafisa wengine ngazi ya Mkoa.
![]() |
| Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Cde Stanley Mkandawire, akiwa na viongozi waliompokea baada ya kuwasili. |
![]() |
| Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Cde Stanley Mkandawire, akizungumza na viongozi katika mkutano uliofanyika Ofisi ya CCM tawi la Tandale Kibaoni. |










No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇