Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa halmashauri kuu ya (CCM) Taifa Mohamed Mchengerwa (MNEC) ambaye pia ni Waziri wa afya wakati wa kufungua mafunzo maalumu kwa madiwani wa CCM Mkoa wa Pwani ambayo yamefanyika katika shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Nyerere iliyopo eneo la kwa mfipa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
Mchengerwa amesema kwamba mafunzo hayo kwa madiwani wa Mkoa wa Pwani watawajengea uwezo mkubwa katika suala zima la kuwatumikia wananchi wao ikiwemo kusikiliza kero na changamotto mbali mbali ambazo zinawakabili wanapaswa kuwa wazalendo.
Kadhalika Mchengerwa amesema kwamba madiwani wanapaswa kuabdilika na kuwa mstari wa mbele katika kwenda kuwa suluhisho katika kuwasikiliza wananchi na kushirikiana nao katika mambo mbali ya kijamii.
"Kwanza kabisa nipende kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati kabisa Katibu wa chama caha mapinduzi (CCM) kwa kuweza kuwakutanisha kwa mara ya kwanza madiwani wote wa CCM wa Mkoa wa Pwani kwa hivyo kitu kikubwa ninachowaomba ni kuwa wazalendo na nchi yao na kuelekeza nguvu zao katika kutatua kero na changamoto za wananchi,"amebainisha Mchengerwa.
Pia Mchengerwa hakusita kugusia suala la madiwani hao kuwa na upendo, na mshikamano wa pamoja katika maeneo yao kwa lengo la kuweza kushirikiana bega kwa bega na wananchi kwa ajili ya kuweza kuwaletea maendeleo chanya.
Kwa uppande wake Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ndg. Kiite Mfilinge amesema kwamba lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwakutanisha madiwani hao ili kuwajengea uwezo ikiwa pamoja na kuwakumbushia kutekeleza majukumu yao pamoja na kuwahudumia wananchi.
Katibu huyo amefafanya kwamba katika mafunzo hayo jumla ya madiwani wote wapatao 185 wameweza kupata fursa ya kushiriki na kwamba wamejifunzo mada mbali mbali ikiwemo suala la uzalendo, uwajibikaji, ulinzi na usalama ikiwa pamoja na kuwa na dira ya pamoja katika ngazi ya Mkoa ambayo itaweza kuleta matokeo ya namna bora ya kuwatumikia wannchi.
Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya uongozi mwalimu Julias nyerere Profesa Mercellina Chijoriga ambaye pia alikuwa mtoa mada katika mafunzo hayo amesema amebainisha kuwa mafunzo hayo yataweza kuleta tija zaidi ya uwajibikaji katika suala zima la kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
Pia Profesa huyo ametumia mafunzo hayo kuwahimiza madiwani wa Mkoa wa Pwani kuzingatia kwa weledi na ufanisi mkubwa dira ya Taifa ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ikiwemo suala zima la utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Nao baadhi ya madiwani ambao wamehudhuria katika mafunzo hayo akiwemo Ally Simba Diwani wa Kata ya Misusugu pamoja na Diwani wa Kata ya Mwewe omary Msombwe wameahidi kwenda kuyatumia vema mafunzo hayo ambayo wameyapata na kwamba yameweza kuwajengea uwezo mkubwa katika kutekeleza majukumu yao.
Mafunzo hayo ya siku moja yamewajumuisha madiwani wote wa Mkoa wa Pwani waoatao 185 ambapo wamepata fursa ya kujifunz amada mbali mbali ikiwemo suala la uzalendo, ulinzi na amani, uwajibikaji kwa wananchi wao , jinsi ya kusimamia mapato, na kujifunza mambo mbali mbali amabyo yataweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika maeneo yao,




No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇