LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 24, 2026

LEKIDEA WATOA NENO LA SHUKRANI KWA MBUNGE ENOCK KOOLA WA VUNJO

 Kwa niaba ya viongozi, wanachama na wadau wote wa maendeleo wa LEKIDEA (Legho Kirua Development Association), tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa Enock Koola (MB), Mbunge wa Jimbo la Vunjo, kwa uongozi wake makini na jitihada kubwa alizoendelea kuzifanya katika kusukuma mbele ajenda za maendeleo ya wananchi wa Kata ya Kirua Vunjo Mashariki na Jimbo la Vunjo kwa ujumla.


Tunathamini kwa kiwango cha juu namna Mheshimiwa Mbunge alivyofanikisha na kuratibu vikao vya LEKIDEA na viongozi wakuu wa Serikali pamoja na taasisi zake Jijini Dodoma tarehe 18 Juni 2026. Kupitia vikao hivyo, ajenda muhimu za maendeleo ziliwasilishwa na kupokelewa kwa uzito unaostahili.

Tunatoa shukrani maalum kwa ushirikiano aliouonesha katika kuendeleza ajenda za:

- Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kirua Vunjo Mashariki;
- Uboreshaji wa Barabara ya Uchira–Kisomachi–Kolarie;
- Mradi wa Bwawa la Urenga kwa ajili ya umwagiliaji na shughuli nyingine za kiuchumi.

LEKIDEA inaamini kuwa ushirikiano huu kati ya viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo na wananchi utaendelea kuzaa matokeo chanya na kuharakisha maendeleo ya Kata ya Kirua Vunjo Mashariki na Jimbo la Vunjo kwa ujumla.

Tunakupongeza Mheshimiwa Mbunge kwa moyo wako wa kujitolea, uwajibikaji na utayari wa kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi. Tunakuahidi kuwa LEKIDEA itaendelea kuwa mshirika mwaminifu wa maendeleo katika kutekeleza miradi yenye manufaa kwa jamii.

Mwenyezi Mungu akubariki, akupe afya njema na hekima zaidi katika kuwatumikia wananchi wa Vunjo.

Ahsante sana Mheshimiwa Mbunge.

Isidori Msaki
Mwenyekiti
LEKIDEA (Legho Kirua Development Association)

Kirua Vunjo Mashariki
22 Juni 2026

Viongozi wa LEKIDEA wakiwa bungeni Dodoma Juni 18, 2026 kwa mwaliko wa Mbunge wao Koola.

 Viongozi wa Lekidea wakitambulishwa bungeni.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages