LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 8, 2026

RAIS SAMIA AAGIZA KUBANWA KWA MATUMIZI YA MAFUTA SERIKALINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza hatua za makusudi za kupunguza matumizi ya nishati ya mafuta katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Katika maelekezo hayo yaliyotolewa leo Ikulu Chamwino, mambo makuu yaliyosisitizwa ni:

✅ Usafiri wa Pamoja: Watendaji wa Ofisi ya Rais na taasisi nyingine za Serikali kutumia usafiri wa pamoja (mabasi madogo) kwenye safari za kikazi badala ya magari mengi.

✅ Udhibiti wa Soko: Wafanyabiashara wameonywa kutoitumia fursa ya kupanda kwa bei ya mafuta duniani kupandisha bei za bidhaa kiholela.

✅ Hali ya Akiba: Nchi ina akiba ya mafuta inayotosheleza mahitaji kwa takribani miezi mitatu, huku serikali ikiendelea kufuatilia mwenendo wa bei ili kumlinda mwananchi.

Hatua hizi zinakuja kufuatia athari za vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati ambavyo vimesababisha kupanda kwa bei ya nishati duniani.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages