Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, amefanya mazungumzo mazito na Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, jijini Kampala kuhusu hatma ya amani nchini Sudan Kusini.
Dkt. Kikwete amemtembelea Museveni akiwa katika jukumu lake jipya kama Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) kwa Ukanda wa Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu. 🛡️
Mambo makuu kutoka kwenye mazungumzo hayo:
✅ Msimamo wa Uganda: Rais Museveni amesisitiza kuwa Uganda iko tayari kulinda amani na maridhiano Sudan Kusini ili kuimarisha uchumi wa ukanda wetu.
✅ Suluhu ya Mezani: Viongozi hao wamekubaliana kuwa amani ya kudumu itapatikana tu ikiwa pande zinazovutana zitakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo.
✅ Uzoefu wa Dkt. Kikwete: Uteuzi wa Dkt. Kikwete unatajwa kuwa chachu ya kuleta "suluhu za Kiafrika kwa matatizo ya Waafrika" kutokana na rekodi yake ndefu ya diplomasia.
Amani ya Sudan Kusini ni amani ya Afrika Mashariki nzima! 🇹🇿🇺🇬🇸🇸




No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇