LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 12, 2026

MZINDAKAYA ATAKA RUKWA IONGEZEWE MADAKTARI, NRFA IONGEZE KIWANGO CHA UNUNUZI WA MAZAO

 


 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Mhe. Jacqueline Mzindakaya ametoa mchango wenye tija akimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mapinduzi makubwa ya afya mkoani kwetu, ikiwemo: ✅ Kupungua kwa vifo vya akina mama wajawazito (kutoka 128 hadi 60). ✅ Kupungua kwa vifo vya watoto wachanga (kutoka 11 hadi 7). ✅ Ujenzi wa Hospitali 4 za Wilaya, vituo vya afya 39, na zahanati 219. Hata hivyo, ameiomba Serikali kuongeza watumishi wa afya (madaktari wa upasuaji wa wanawake wajawazito) katika Hospitali ya Wilaya ya Kalambo inayokabiliwa na upungufu wa watumishi kwa 70% . Pamoja na ujenzi wa barabara ya kuelekea Kituo cha Afya Kasu, Wilaya ya Nkansi . Akiwasemea wananchi wa Rukwa, Mzindakaya amesisitiza Malipo ya haraka kwa wakulima kupitia NFRA, Pia NFRA kuongeza kiwango cha ununuzi wa mazao kulingana na kasi kubwa ya uzalishaji, Ukamilishaji wa skimu ya umwagiliaji ya Katongolo (Nkansi) na kuongeza skimu nyingine za Umwagiliaji mkoani Rukwa.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages